BANGAIZA NA MREMA KUWANIA MATAJI YA NDONDI YA WBA KESHO NCHINI AUSTRALIA. - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BANGAIZA NA MREMA KUWANIA MATAJI YA NDONDI YA WBA KESHO NCHINI AUSTRALIA.

Na Asha Said, DAR ES SALAAM
MABONDIA wawili wa Tanzania, Suleiman Bangaiza na Goodluck Mrema leo wamepima uzito kwa ajili ya mapambano yao yatakayofanyika kesho ukumbi wa Seagulls Rugby League Club, Tweed Heads mjini New South Wales nchini Australia.     
Akizingumza kwa simu kutoka New South Wales, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania  (PST), Anthony Ruta amesema Mrema atazipiga na Jason Moloney wa Australia kugombea ubingwa wa Chama cha Ngumi Duniani (WBA) uzito wa Bantam katika pambano la Raundi 10.
Suleiman Bangaiza (wa pili kushoto) akiwa na mpinzani wake, Andrew Moloney wakati wa kupima uzito 
Suleiman Bangaiza na Goodluck Mrema katika picha ya pamoja na wapinzani wao baada ya kupima uzito

Ruta ambaye naye ni bondia wa zamani wa kimataifa, amesema kwa upande wake Bangaiza atazipiga na bingwa wa WBA Oceania, Andrew Moloney katika pambano la uzito wa Super Fly.
Rutta amesema kwamba wanashukuru wamefika salama nchini humo na kesho mabondia hao wapo tayari kwa mapambano ha... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More