Barack Obama aja kimya kimya Tanzania na kuacha ujumbe mzito serikalini (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Barack Obama aja kimya kimya Tanzania na kuacha ujumbe mzito serikalini (+video)

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama leo Julai 5, 2018 ameondoka nchini Tanzania baada ya kutimiza ziara yake ya kimya kimya ya mapumziko katika Hifadhi za Taifa za Serengeti zilizopo mkoani Mara.


Barack Obama na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga akimlaki Obama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) amesema kuwa Obama alikuja nchini siku 8 zilizopita na yeye ndiye aliyempokea lakini Rais huyo mstaafu hakutaka taarifa zisambae kwani alihitaji awe faragha zaidi.


Kwa upande mwingine, Mkuu wa Moa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira amesema kuwa kwa dakika moja aliyoongea naye, Obama amesema Serikali lazima ijitahidi kuvitangaza vivutio vyake kimataifa kwani, inavivutio vingi sana lakini watu hawavijui. Tazama video hapa chini akilakiwa


The post Barack Obama aja kimya kimya Tanzania na kuacha ujumbe mzito serikalini (+video) appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More