Barakah The Prince Adaiwa Kabadili Dini Kisa Mpenzi Wake Naj - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Barakah The Prince Adaiwa Kabadili Dini Kisa Mpenzi Wake Naj

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amethibitisha taarifa za yeye kubadilisha dini lakini inadaiwa amebadilisha dini kwa ajili ya mpenzi wake Naj.


Barakah ambaye alikuwa muumini ya dini ya kikristo amesemekana kubadilisha dini na kuhamia katika imani ya Kiislamu kwa ajili ya mpenzi wake Naj ambaye ni muislamu pia.


Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni na kituo kimoja cha habari Barakah amethibitisha kuwa amebadilisha dini yake:Ujue mambo ya dini bro ni imani, sio rahisi kama wengine wanavyochukulia hivyo mpaka unaikana imani unakua umeamua sana, umefatilia umejua faida na hasara zake“.Ingawa Barakah hajaweka wazi sababu kabisa ya kubadilisha dini yake lakini inasemekana amefanya hivyo ili aweze kumuoa mpenzi wake Naj ambaye tayari ni muislamu.


The post Barakah The Prince Adaiwa Kabadili Dini Kisa Mpenzi Wake Naj appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More