Baraza la Ardhi jijini Arusha larejesha ekari 15 kwa Wananchi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Baraza la Ardhi jijini Arusha larejesha ekari 15 kwa Wananchi

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
BARAZA la Ardhi na Nyumba wilaya ya Arusha limetengua umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa hekari 15 iliyokuwa ikimiliwa na mwanajeshi mstaafu,Willison Rugumam aliyejenga kituo cha watoto yatima cha Huruma Vision Tanzania na kulirejesha kwa wananchi wa kata ya Sokoni one katika Jiji la Arusha.
Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita ,katika kesi ya Ardhi Namba 147 ya mwaka 2012 iliyofunguliwa na Rugumam akiwalalamikia wananchi saba wa kata ya Sokon I kwa kuvamia eneo hilo na kufanya uharibifu ,mwenyekiti wa baraza hulo,Fadhili Mdachi alidai kuwa mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha uhalili wa yeye kuwa mmiliki wa eneo hilo hivyo baraza limetupa maombi yake.
Mdachi amesema kuwa Rugumam alipeleka maombi ya kutaka baraza hilo limtambue yeye kama mmiliki halali wa eneo hilo lakini ushahidi alioutoa kupitia mashahidi wake saba umekosa mashiko ya kulishawishi baraza hilo limtambue kama mmiliki halali wa eneo hilo.
Katika hukumu hiyo ,Mdachi alizingatia ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More