Barnaba Amtabiria Haya Hamisa Mobetto - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Barnaba Amtabiria Haya Hamisa Mobetto

STAA wa Bongo Fleva, Elias Barnaba, 'Barnaba Classic' amemtabiria mafanikio makubwa mwanamitindo mahiri nchini, Hamisa Mobetto, aliyeamua kujitosa kwenye muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’.Kauli ya Barnaba imekuja siku chache baada ya baadhi ya watu kumponda Mobetto waliosema mlimbwende huyo anakwenda kuangukia pua kwa kuwa hana kipaji cha muziki.

Akizungumza na DIMBA, Barnaba, alisema anamwona Mobetto ana kipaji ambacho kikiongezewa kitu kidogo muziki wake utafika mbali na ya kuja kushindanishwa na wasanii wenye majina makubwa kwa sasa.

“Ukimzungumzia Hamisa naona ana mafanikio makubwa sana huko mbeleni, alianza na mitindo na sasa namwona katika nafasi nyingine ya kujitambulisha kupitia muziki, ninachomshauri asisikilize maneno ya watu akaze buti na kufanya kazi,” alisema Barnaba.
... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More