“BASATA Mnaua Sanaa, Ubunifu na Vipaji”- Roma - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“BASATA Mnaua Sanaa, Ubunifu na Vipaji”- Roma

Msanii wa muzili kutoka kundi la ROSTAM, Toma Mkatoliki amewatolea uvivu Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) baada ya kufungiwa nyimbo yao mpya.


Roma Mkatoliki amemwaga povu hilo baada ya ya yeye na msanii mwenzake Stamina kufikishwa BASATA siku ya jana baada ya kuachia wimbo wao wa Parapanda.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Roma ameandika na kudai kuhuzunishwa na jinsi BASATA wamekuwa wakifanya maamuzi yao juu ya kazi za wasanii.


Roma ameandika kuwa BASATA inaua Sanaa, Ubunifu na vipaji na kudai hachukizwi na BASATA bali anachukizwa na utendaji kazi wao pia akawataka mashabiki zake watoe maoni huku akisisitiza haoni kama wimbo wao wa parapanda ulikuwa na sababu za kufungiwa.The post “BASATA Mnaua Sanaa, Ubunifu na Vipaji”- Roma appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More