BASATA Wakanusha kuifungia Parapanda. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BASATA Wakanusha kuifungia Parapanda.

Katika ukurasa wake wa Twitter Roma Mkatoliki aliandika wiki iliyopita na kusema baraza la sanaa tanzania linaua vipaji na muziki wa tanzania kwa kile wanachokuwa wakikifanya , hii ni post iliyoandika na roma ikiwa ni kama siku tatu tu tangu walipotoa wimbo wao uliokwenda kwa jina la Parapanda.


Hata hivyo baada ya hapo wikiendi yote iliyopita , habari ziliozkuwepo katika mitandao ya kijamii na vyomba vya habari ni kwamba wimbo wa parapanda umefungiwa na BASATA , huku ikisemakana kuwa wasanii hao waliitwa kuhojiwa kuhusu wimbo wao.


Sasa basi , BASATA wamefunguka na kuongelea trending news ya parapanda na kusema kuwa habari zinazosambaa kuwa wasnaii hao wameitwa basata sio kweli na hakuna kitu kama hicho labda wawe wanatafura kiki.


BASATA wansema kuwa waanii hao watakuwa wameamua kujifungia wimbo huo kwa nia ya kutafuta kiki na kuuza wimbo huo lakini wao kama baraza hawajawaita wasanii ROMA  na STAMINA kama ilivyokuwa imeripotiwa.


The post BASATA Wakanusha kuifungia Parapanda. appeared... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More