BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/- - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/-

Na Khadija Seif,Globu ya jamii  .    BARAZA la Sanaa Tanzania(BASATA) limewatoza faini ya Sh.milioni tatu kila mmoja Msanii Raymond Mwakyusa a.k.a Rayvanny na Naseeb Abdull maarufu Diamond pamoja na lebo ya WCB baada ya kukaidi kuufuta wimbo wao wa Mwanza kwenye Youtube.
Kwa mujibu wa BASATA ilitoa tamko kwa wasanii hao wanaotoka lebo la WCB kuufuta wimbo huo jana kabla ya saa 10:30 jioni na kutochezwa redioni na kwenye luninga lakini hawakufanya hivyo.
Katibu Mtendaji wa  BASATA Godfrey Mngereza amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa bado anasisitiza kuondolewa kwa wimbo  kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu za baraza hilo kwani ndio wasimamizi wakuu wa kazi za sanaa nchini .
Mngereza  ametoa rai kwa vyombo vyote,mitandao ya kijamii,watu ,pamoja na kumbi za starehe kutotumia wimbo huo kwani umeshafungwa rasmi toka siku ya jana.
Kwa upande wa Meneja wa Lebo hiyo ya WCB Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella amesema wamepokea taarifa hizo na kukubaliana nao kuwa ifike pahala wasani... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More