BASATA YAUTAKA UONGOZI WA WCB KUFUTA WIMBO WA 'MWANZA' KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KABLA YA SAA KUMI KAMILI JIONI LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BASATA YAUTAKA UONGOZI WA WCB KUFUTA WIMBO WA 'MWANZA' KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KABLA YA SAA KUMI KAMILI JIONI LEO

Na Agness Francis, blogu ya Jamii
BARAZA la sana Taifa (BASATA) limeufungia rasmi leo Novemba 12 mwaka huu wimbo Ujulikanao kwa jina la Mwanza ulioimbwa na msanii wa lebo ya Wasafi Raymond Mwakyusa, maarufu Kama Rayvanny. 
Ambapo wimbo huo wa Mwanza alimshirikisha msanii mwenzake Naseeb Abdul (Diamond Platinumz). 
Amesema hayo Katibu wa baraza la sana Taifa Geofrey Mngereza kuwa baraza limeamua kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji wa maadili ya kitanzania kwa msanii Rayvanny kutumia maneno yanayohasisha ngono katika wimbo huo. 
Mgereza amesema pamoja na kuufungia wimbo huo baraza linawaonya wasanii hao, vyombo vya habari ama mtu yoyote kutoutumia kucheza au kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. 
"Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria la Baraza namba 23 ya mwaka 1984 na kanuni zake limepewa mamlaka ya kusimamia Sanaa, wasanii na mtu yoyote anayejishughulisha na kazi za sana hapa Nchini"amesema Mngereza. 
Katibu huyo amesema kuwa Baraza hilo linatoa onyo kali kwa msanii Rayv... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More