BASI LA MWENDOKASI LAPATA AJALI MAGOMENI MAPIPA JIJINI DAR ES SALAAM IJUMAA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BASI LA MWENDOKASI LAPATA AJALI MAGOMENI MAPIPA JIJINI DAR ES SALAAM IJUMAA

Dereva wa gari dogo aina ya Nissan March lenye namba za usajili T968 DNZ amefariki dunia baada ya gari hilo kugongana na Basi la Mwendokasi eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es salaam mchana wa Ijumaa Kuu. 

Kwa mujibu wa mashuhuda, basi la mwendokasi lilikuwa likitoka maeneo ya Kariakoo kwenda Kimara, kabla ya kuligonga gari hilo dogo ambalo liliklatika katikati huku dereva wake akifariki dunia papo hapo.

Shuhuda wanasema mwenye gari dogo alikuwa anakata kona kutoka Magomeni kwenda Kariakoo, sasa wakati anataka kuikata kona katika taa ndogo za kuongoza magari za Magomeni Mapipa ambazo zilikuwa haziwaki ndipo gari dogo ikachelewa kupita na mwendokasi likawa limefika na kuligonga.
Vipande viwili vya gari hilo vimechukuliwa na kupelekwa kituo cha Polisi Magomeni huku mwili wa dereva huyo ambaye haujafahamika jina lake umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More