BATENGA PEKEE AREJESHWA KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SC, MWENYEKITI MPYA LYAMWIKE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BATENGA PEKEE AREJESHWA KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SC, MWENYEKITI MPYA LYAMWIKE

Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM
MWANACHAMA  maarufu wa Simba SC, Issa Batenga ataendelea kuwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, kufuatia kuteuliwa tena na Bodi ya Muda ya Wakurugenzi ya klabu hiyo Jumapili.
Taarifa ya Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, imesema kwamba Bodi hiyo imeteua kamati ya uchaguzi ya watu watano kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo, chini ya Mwenyekiti, Boniphace Lyamwike na Makamu wake, Wakili Steven Ally.
Issa Batenga anakuwa mtu pekee kutoka Kamati iliyopita ya Uchaguzi ya klabu hiyo kuwemo kwenye Kamati mpya na bahati nzuri anaendeleka na majukumu yale yale ya Ukatibu.
Issa Batenga (kushoto) ataendelea kuwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC 

Wajumbe wawili walioteuliwa kuungana na Lyamwike, Wakili Steven na Batenga ni Iddi Mbita na Richard Mwalwiba.
Salim amesema kwamba Kamati hiyo itatangaza tarehe ya uchaguzi hivi karibuni na kuitisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Simba SC (Simba Sports Club Co... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More