BBC yazindua kipindi kipya cha afya ‘BBC Maisha’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BBC yazindua kipindi kipya cha afya ‘BBC Maisha’

BBC Maisha kipindi kipya cha Afya kinazinduliwa wiki hii kwenye runinga yako, na kinaangazia masuala ya afya ambayo mara nyingi huonekana kama mwiko, japo yanaendelea kuathiri jamii Barani Afrika. Kipengele cha kwanza kwa jina FUNGUKA kinatoa nafasi wachangiaji na jamii nzima kufungua siri zao katika maisha ambazo mara nyingi zinagusa afya na maisha yao .Makala ya kwanza yanaagazia utamaduni wa kuwakeketa wanawake na wasichana . Ni suala muhimu sana hususan msimu huu wa likizo ndefu, ambayo kuna mambo mengi yanafanyika katika jamii, moja wapo ni watoto kupelekwa jandoni, baadhi ya jamii zikiwakeketa wasichana wao. Makala mengine yajao yataangazia tatizo la kutoa/kuavia mimba, Sonanoa, Huzuni, uraibu wa mihadarati, na unyaji pombe wa kupindukia.


Mtangazaji nyota wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Maryam Dodo Abdullah ndiye anayeongoza mazungumzo ya FUNGUKA, akiwa na ufasaha wa lugha na uwelewa masuala ya afya hususan kanda ya Afrika Mashariki.


Mhariri wa kipindi cha BB... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More