Bei ya Mafuta yahofiwa kuongezeka duniani - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Bei ya Mafuta yahofiwa kuongezeka duniani

Vyombo vya habari vinavyojishughulisha na masuala ya uchumi duniani kama vile gazeti la Financial Times na televisheni ya CNBC vimesema kuwa, huenda bei ya mafuta ikapanda vibaya kwa hadi dola 10 kwa pipa, baada ya ndege zisizo na rubani za jeshi la Yemen kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya taasisi kubwa zaidi ya mafuta a Saudi Arabia.


Shambulio la ndege 10 zizizo na rubani za Jeshi na Kamati za Kujitolea za Wananchi wa Yemen limeilazimisha Saudi Arabia kukata nusu nzima ya uzalishaji wake wa mafuta.


Taarifa rasmi kutoka Serikali ya Saudi Arabia inasema kuwa nchi hiyo imepoteza uwezo wa kuzalisha mapipa milioni tano na laki saba kwa siku, yaani nusu nzima ya uzalishaji wake. Hata hivyo wataalamu wa mambo wanasema kuwa, bado ni mapema mno kujua hasara hasa iliyopata Saudi Arabia kutokana na shambulio hilo ambapo hasara hizo zinaonekana ni kubwa mno ikilinganishwa na takwimu zinazotolewa na Serikali ya Saudia.


Mkuu wa taasisi ya mafuta la Lipow Pil Associates ya Marekani, An... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More