BEKI WA KATI JOB IBRAHIM WA NDANDA FC ALIYEWAHI KUCHEZEA YANGA SC ASAINI LIPULI FC - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BEKI WA KATI JOB IBRAHIM WA NDANDA FC ALIYEWAHI KUCHEZEA YANGA SC ASAINI LIPULI FC

Na Mwandishi Wetu, IRINGA
TIMU ya soka ya Lipuli FC ya mkoani Iringa imeendelea kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao, baada ya kumsaini beki wa Ndanda FC ya Mtwara, Job Ibrahim.
Job, mlinzi hodari wa katikati aliyewahi pia kuchezea Yanga SC, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na kikosi cha kocha Suleiman Abdallah Matola.
Job anafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Lipuli FC kufika watano baada ya kiungo, William Lucian ‘Gallas’ kutoka Ndanda FC pia, washambuliaji Miraj Madenge ‘Shevchenko’ kutoka Mwadui FC, Paul John Nonga kutoka Mwadui FC ya Shinyanga ambao wote kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Issa Ally Rashid, mchezaji huru aliyesaini mkataba wa miaka miwili.
Job Ibrahim (kushoto) wakati anasaini Lipuli FC jana mjini Iringa
  

Gallas na Shevcheko wanakwenda kuungana tena na Suleiman Matola, aliyekuwa kocha wao kuanzia timu ya vijana ya Simba SC chini ya umri wa miaka 20, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013 na baadaye kuchwa mwaka 2014.
Na N... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More