Ben Pol Ajibu Tuhuma Za Kupotea Kimuziki na Mziki Mpya - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ben Pol Ajibu Tuhuma Za Kupotea Kimuziki na Mziki Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na mahadhi yake RnB, Bernard Paulo maarufu kama Ben Pol ametangaza kuja na staili mpya ya muziki baada ya Tetesi za kupoteza ladha katika mziki wake.


Mashabiki wa Ben Pol wamedaiwa kulalamika Msanii huyo kupoteza muelekeo katika hii miaka ya katibuni na kuishia kupoteza muziki ambao hauna ladha ya kuvutia kama ilivyokuwa zamani.


Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ben Pol ameweka wazi kuwa yeye hajabadilika kama msanii bali somo ndio limebadilika pia amedai kuwa anataka kuwafurahisha hao wanaodai amepotea kwa mziki mpya:Wanaosema hivyo ntawafurahisha very soon”.Lakini mbali na kuzungumzia hilo ametaja kolabo zake alizofanya na wasanii kutoka nje mfano kolabo zake na wasanii wa Nigeria kuwa zimesaidia sana kwani zimemueka sehemu nzuri ambayo anafanya vizuri katika baadhi ya nchini za kiafrika hasa kwa upande wa Afrika mashariki na Afrika magharibi.


The post Ben Pol Ajibu Tuhuma Za Kupotea Kimuziki na Mziki Mpya appeared first on Ghafla!Ta... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More