Ben Pol atupilia mbali tetesi kuhusu Darassa na dawa za kulevya, ‘Kusema kweli siamini’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ben Pol atupilia mbali tetesi kuhusu Darassa na dawa za kulevya, ‘Kusema kweli siamini’

Msanii wa muziki Bongo, Ben Pol amefunguka kuhusu tetesi zinazodai kuwa rapper Darassa ametumbukia kwenye matumizi ya dawa ya kuelewa.


Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Zai’ ameiambia Clouds TV kuwa kitu hicho bado hakiamini kwani amekuwa  akiwasiliana na Darassa mara kwa mara.


“Kusema kweli siamini, sina element yoyote inayonifanya niamini chochote kuhusiana na hizo tetesi kwa sababu ili mtu uweze kusema kitu lazima uwe na element ambazo umeziona lakini mimi hamna element,” amesema.


“Mimi tunaongea masaa mawili, saa zima kwenye simu, video call sometime kwa hiyo sioni kuna element ya hicho kitu,” ameongea.


Darassa amemshirikisha Ben Pol katika nyimbo mbili ambazo ni Sikati Tamaa na Muziki, huku Ben Pol akimshirikisha Darassa katika ngoma moja, Tatu.

Loading...Jiunge na Bongo5.com sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kal... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More