BENKI KUU YA TANZANIA YAPONGEZA UBUNIFU WA BENKI YA NMB KATIKA KURAHISHA HUDUMA ZA KIBENKI NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI KUU YA TANZANIA YAPONGEZA UBUNIFU WA BENKI YA NMB KATIKA KURAHISHA HUDUMA ZA KIBENKI NCHINI


*Yazindua huduma ya Klik App NMB inayowezesha kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeipongeza Benki ya NMB kwa uamuzi wake wa kuzindua huduma ya kufungua akaunti kwa kutumia mtandao wa simu ya mkononi.Imesema hatua hiyo imethibitisha namna benki hiyo inavyotumia ubunifu na kukua kwa teknelojia ya mawasiliano kwa kurahisisha huduma za kibenki nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese wakati akizindua Klik App ya NMB inayowezesha mteja kufungua akaunti kupitia simu ya kiganjani.

Amesema kuwa ubunifu huo ambao umefanywa na benki ya NMB utarahisha watanzania wengi kufungua akaunti za benki hiyo kupitia simu zao na kwamba hivi sasa watumiaji wa simu za mkononi ni wengi na hivyo huduma hiyo ya NMB imekuja wakati sahihi.

“Tunaipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao wa kuhakikisha wanatumia teknolojia iliyopo kuanzisha huduma za kufungua akaunti kupitia simu ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More