BENKI KUU YAFAFANUA KUHUSU USIMAMIZI KWA WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI KUU YAFAFANUA KUHUSU USIMAMIZI KWA WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetoa tangazo kwa umma kupitia tovuti yake (www.bot.go.tz) likiwataka watu na taasisi zote zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha zilizoko Tanzania Bara (isipokuwa vyama vya ushirika vya
akiba na mikopo – SACCOS) kutoa taarifa zitakazotumika katika utayarishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Usimamizi wa Maduka ya Fedha na Huduma Ndogondogo za Fedha Victor Tarimu kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT).Tarimu amesema taarifa hizo zinatakiwa kutumwa Benki Kuu ya Tanzania hadi 31 Januari 2019 na kwamba inatoa ufafanuzi ufuatao kuhusu tangazo hilo kuwa lengo la siyo kuvifunga au kuvibana vikundi vya kijamii kama VICOBA, watu binafsi na taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha kama ambavyo inapotoshwa na baadhi ya watu na mitandao mbalimbali ya kijamii.

"Bali ni kukusanya taarifa za awali kuhusu huduma hizo, kama amnavyo ilivyoai... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More