BENKI YA AMANA WAZINDUA MIKOPO YA VIKUNDI KWA WAJASIRIAMALI WADOGO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA AMANA WAZINDUA MIKOPO YA VIKUNDI KWA WAJASIRIAMALI WADOGO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BENKI ya Amana imeadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuzindua rasmi mikopo ya vikundi ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutimiza azma ya kuwafikia na kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini. 
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dr Muslim Masoud amesema kuwa, mikopo hiyo ya vikundi itawawezesha wananchi wa kipato cha chini kujikwamua kiuchumi kama wanavyoendelea kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kuwapa mikopo inayoanzia milioni moja hadi kumi. 
Dr Masoud amesema kuwa, mpaka sasa wameshatoa mkopo wa Bilioni 143 kwa wateja wakubwa , wakati na wadogo na wakisaidia kuwainua kiuchumi wajasiriamali wengi na wafanyabiashara wadogo."Benki ya Amana inatimiza miaka saba na mpaka leo tumetoa mikopo ya Bilioni 143 kwa wateja wote wakiwa wameweza kutimiza azma ya kuwafikia na kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini,"amesema Dr Masoud.
Amesema kwa wajasiriamali wadogo watatakiwa kuwa kwenye vikundi na sio mmoja mmoja nanwakiw... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More