BENKI YA AZANIA YAWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE UBORA WA HUDUMA BAADA YA KUINUNUA 'BANK M' - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA AZANIA YAWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE UBORA WA HUDUMA BAADA YA KUINUNUA 'BANK M'

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya hatua ya benki yake kuinunua Bank M.

Benki ya Azania leo imewahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kutoa huduma za ubora wa hali ya juu kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa kipindi kirefu sasa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari. Hii ni baada ya Benki kuu ya Tanzania (BoT) kutoa tamko kuhusiana na kukamilika rasmi kwa mchakato wa kuhamishia Mali na Madeni ya iliyokuwa Benki M na kuzihamishia benki ya Azania 
Tumeingia kwenye makubaliano na BoT ya kuinunua benki M ya Dar es Salaam hatua ambayo itapanua soko letu katika sekta ya kifedha hapa nchini Tanzania. Ununuzi huu wa benki M unatarajiwa kuongeza ufanisi kupitia michakato iliyoboreshwa, utamaduni na kuongeza soko. Itembe amesema. 
Mnamo Agosti 2018, BoT iliiweka benki M chini ya uangalizi maalum kutokana ... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More