Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro

Benki ya Biashara Mkombozi imezindua rasmi Tawi la Morogoro ambalo limepandishwa hadhi kutoka kituo cha huduma za kifedha na sasa kuwa tawi kamili.
Zoezi hili linafanyika wiki moja tu baada ya Benki ya Biashara Mkombozi kuzindua Tawi la Tegeta ambalo pia lilikuwa kituo cha cha huduma za kifedha hapo awali.
 Ufunguzi wa Tawi hilo ulifanywa na Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro Bi. Ruth John akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa,  wadau mbalimbali, wafanyakazi, wafanyabiashara na wateja wa Benki ya Biashara Mkombozi.
 Akizindua tawi hilo jipya, mgeni rasmi aliipongeza Benki ya Biashara Mkombozi kwa hatua iliyofikia na kusema uzoefu kutoka nchi nyingine unaonyesha kuwa wafanya biashara wadogo na wale wakati ni wadau muhimu sana katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini.
“Hivyo napenda kuwapongeza benki ya Biashara Mkombozi kwa kuamua kuwafikia wadau hawa muhimu ambao baadhi ya taasisi za kifedha zinawatizama kama ni soko hatarishi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More