Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua tawi la Tegeta - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua tawi la Tegeta

Na Mwandishi wetu,Benki ya Biashara ya Mkombozi imezindua rasmi Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam baada ya tawi hilo kupanda hadhi kutoka kituo cha huduma za fedha na sasa kuwa tawi kamili.
Tawi hilo lilifunguliwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali, wafanyakazi na wateja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi.
Akizindua tawi hilo jipya, Askofu Nzigilwa alisema benki inaendelea kukua vizuri kama ilivyotarajiwa na kwamba malengo ya Benki ya Biashara ya Mkombozi ni kuwa na matawi nchi nzima ili Watanzania wote waweze kupata huduma za kibenki.
“Nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuitumia  benki hii. Hii ni benki  inayomilikiwa na Watanzania wenyewe kwani mpaka sasa hakuna pesa yeyote iliyowekwa na mwekezaji yeyote wa nje,” alisema na kuongeza kuwa ufunguzi  wa tawi hilo la Tegeta ni udhihirisho wa dhamira njema ya Benki ya Mkombozi kama mdau muhimu katika uchumi na maendeleo ya sekta ya fedha.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More