Benki ya CRDB yakabidhi Milioni 20 katika Hospitali ya Sekou Toure Jijini Mwanza - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Benki ya CRDB yakabidhi Milioni 20 katika Hospitali ya Sekou Toure Jijini Mwanza

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Benki ya CRDB imekabidhi hundi ya shilingi Milioni 20 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Sekou Toure ili kusaidia ukarabati na ununuzi wa vifaa tiba katika wodi ya upasuaji (Theatre) ya akina mama katika Hospitali hiyo.


Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi hiyo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema benki hiyo ni mdau mkubwa katika kuboresha huduma za afya hapa nchini ambapo imekuwa ikitoa asilimia moja ya faida yake kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Dkt. Bahati Msaki aliishukru Benki ya CRDB kwa mchango huo na kwamba utasaidia kuondoa changamoto ya utoaji huduma za afya kwa akina mama.


Mbali na hundi hiyo, pia Benki ya CRDB ilikabidhi luninga (TV) tatu za kisasa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa, Bugando  ili kutoa huduma kwa wananchi na wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza kw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More