BENKI YA CRDB YATWAA TUZO YA BENKI BORA TANZANIA, 2019 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA CRDB YATWAA TUZO YA BENKI BORA TANZANIA, 2019

Benki ya CRDB imetajwa kuwa benki bora zaidi kwa mwaka 2019 nchini na Shirika la habari la Finacial Times la nchini Uingereza kupitia jarida la 'The Banker', katika hafla maalum ya utoaji tuzo iliyofanyika katika hoteli ya Sheraton Grand Park Lane, jijini London, Uingereza.
Akizungumza kuhusiana na tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela alisema  tuzo hiyo ni kielelezo cha ukuaji ambao benki hiyo imeupata katika mwaka huu wa 2019 ambao kwa kiasi kikubwa unachangiwa na maboresho ya huduma kwa wateja na uwekezaji katika mifumo ya kidijitali ambao umesaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma na kusogeza huduma karibu zaidi na wateja.
"Tunajivunia sana tuzo hii. Kipekee kabisa niwashukuru sana wateja wetu kwa kutuamini na kutupa nafasi ya kuwahudumia. Tuzo hii inatufanya kutambua kuwa tuko katika njia sahihi ya kuwapatia wateja wetu huduma zilizo bora, "alisema Nsekela.
Akizungumza kwa niaba ya jopo la majaji wa tuzo hizo, ambalo linajumuisha wahariri wa Financial Times ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More