BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA

Na.WFM Mjini Bali- Indonesia

Benki ya Dunia imeahidi kuwekeza zaidi nchini Tanzania katika Sayansi na Teknolojia ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa lengo la kuisaidia Tanzania kukuza uchumi wa viwanda na kuondoa umasikini kwa wananchi wa wake.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, alipofanya mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem, katika mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Mjini Bali Indonesia.

Dkt. Mpango amesema kuwa Benki ya Dunia imeamua kuwekeza katika teknolojia kwa kuwa ni eneo sahihi linaloweza kukuza uchumi wa Taifa kwa zaidi ya mara mbili kutokana na tafiti zilizofanywa na Benki ya Dunia.

“Kimsingi Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia amefurahia ajenda za maendeleo za Tanzania kuhusu kujenga uwezo wa rasilimali watu katika kukuza uchumi wa viwanda na ameahidi kuanza kwa kuwekeza zaidi kwa watoto wenye umri mdogo i... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More