Benki Ya Dunia Yaipatia Tanzania Mkopo Wa Trilioni 1 - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Benki Ya Dunia Yaipatia Tanzania Mkopo Wa Trilioni 1

Benki ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 450 sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.035, kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfumo wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, awamu ya tatu.


Tukio hilo limefanyika Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu-Hazina Bw. Doto James na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird.
Bw. James amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kupatikana kwa mafanikio makubwa ya awamu mbili zilizopita kwa kusaidia kaya masikini kwa kuongeza kipato na huduma za kijamii, kiuchumi ikiwemo kuwaendeleza watoto wao.
“Mpango huu katika kipindi cha pili ni kuwezesha kaya masikini kutumia fursa ya kuongeza kipato na huduma za kijamii na kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo ya watoto wao” alisema Bw. James
Alisema malengo mengine yatakuwa ni kutekeleza miradi inayotoa ajira za muda ikihusisha ujenzi wa miundombinu hususan kwenye sekta mahususi kamavile afya, elimu, maji,... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More