Benki ya Exim yazindua kampeni ya ‘Deposit Utokelezee na Exim’ - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Benki ya Exim yazindua kampeni ya ‘Deposit Utokelezee na Exim’


 Benki ya Exim Tanzania leo imezindua rasmi kampeni yake inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na Exim’ ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam leo inawawezesha wateja wa benki hiyo kupata viwango vya riba vya kuvutia hadi asilimia 10.5 ikiwa watafungua akaunti ya amana maalum (fixed deposit) au kuweka kwenye akaunti zao za amana maalum kiasi kisichopungua Sh 50m/- kabla ya Desemba 31 mwaka huu..

"Kampeni hii inalenga kukuza utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa watanzania. Kwa kuzingatia viwango vya ushindani tunavyowasilisha kupitia kampeni hii, wateja wetu watakuwa na uwezo wa kunufaika na riba ya hadi 10.5% kwenye amana zao, " Alisema Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes Kaganda wakati hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kampeni hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More