BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU

Na Agness Francis, Globu ya JamiiBenki ya I & M inaendelea kutoa zawadi kwa wateja wake katika droo  ya pili JIDABO na I & M bank chini ya usimamizi kutoka Bodi ya Taifa  ya Michezo ya Kubahatisha iliyochezeshwa leo ambapo washindi  watano wamepatikana kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini 
Akizungumza na Waandishi wa  Habari leo Jijini Dar es  Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja na reja reja, Ndabu Swere amesema kuwa  promosheni hiyo iliyoanza mwezi Octoba na kuendelea mpaka Disemba kwa kila mwezi kutaja washindi watano wa droo hiyo. 
Ndabu amesema washindi watano waliopatikana leo ni sehemu ya washindi 15 ambao watapatikana katika kipindi chote cha miezi mitatu ya promosheni ya "JIDABO na I&M". Aidha Ndabu amesema kuwa mpaka  sasa wameshapata jumla ya washindi 10 na kubakiza wengine  5 ambao watapatikana katika droo ya mwezi huu
"Ili kuweza kushiriki Promosheni hii mteja anapaswa afungue akaunti ya Akiba, biashara, mtoto katika tawi lolote la Benki ya I & M katika kipindi chote c... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More