BENKI YA MAENDELEO TIB YATOA FEDHA KUSAIDIA UJENZI WA VITUO VYA MABASI MKURANGA NA KAHAMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA MAENDELEO TIB YATOA FEDHA KUSAIDIA UJENZI WA VITUO VYA MABASI MKURANGA NA KAHAMA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

BENKI ya Maendeleo (TIB) imesaini mikataba ya msaada wa kiufundi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga  na Halmashauri ya Mji wa Kahama  na kwa mujibu wa mkataba huo benki ya TIB itatoa jumla ya shilingi 873,000,000 ili kusaidia Halmashauri hizo mbili kulipia gharama za wataalamu washauri watakaofanya upembuzi yakinifu na pia kuandaa michoro na makisio ya gharama na nyaraka za zabuni kwa ajili ya vituo vipya vya mabasi vitakavyojengwa kwenye Halmashauri hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makubaliano hayo Kaimu Mkurugenzi uendeshaji wa Benki ya TIB Patrick Mongela amesema kuwa lengo la mkataba huo ni kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ina manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla, amesema kuwa wao kama Benki hawatoi mikopo pekee pia wanasimamia kikamilifu miradi ya kimaendeleo katika maendeleo ya jamii.
Amesema kuwa katika miradi hiyo Wilaya ya Mkuranga imepata jumla ya shilingi milioni 409.5 na kituo cha mabasi kitajengwa katika kijiji ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More