BENKI YA NMB KUINUA VIJANA KUPITIA MICHEZO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA NMB KUINUA VIJANA KUPITIA MICHEZO


BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vitabu na udhamini wa jezi, mabegi ya michezo na mipira kwa kituo cha vijana cha Don Bosco Upanga cha jijini Dar es Salaam kinachomiliki timu mbili za mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanaume na wanawake ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mchezo huo.

Msaada huo na udhamini wa vifaa hivyo kwa kituo hicho kinachosaidia vijana umegharimu kiasi cha shilingi milioni 15, ambapo akikabidhi Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite alisema benki hiyo itaendelea kuchangia katika shughuli za kusaidia jamii pamoja na kuinua michezo nchini.Akifafaanua katika ufadhili huo, Bw. Ngingite alisema ufadhili huo umejumuisha vitabu mbalimbali kwenye maktaba ya kituo cha Don Bosco Upanga pamoja na vifaa vya michezo vitakavyotumiwa na timu ya mpira wa kikapu wanaume ya Savio na timu ya mpira wa kikapu wanawake ya Lioness zote zikilelewa na kituo hicho.

Alisema NMB imetenga takribani shilingi bilioni moja ikiwa ni maalum kusaidia ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More