BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA STULI NA MEZA ZA MAABARA SHULE YA SEKONDARI MWANTINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA STULI NA MEZA ZA MAABARA SHULE YA SEKONDARI MWANTINI

Benki ya NMB imetoa msaada wa Stuli 32 na meza 8 za maabara zenye thamani ya Shilingi milioni tano ili kusaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi katika shule ya Sekondari Mwantini iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 
Msaada huo umekabidhiwa leo Ijumaa Desemba 6,2018 na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko. 
Katamba alisema msaada huo wa stuli na meza ni sehemu ya ushiriki wa benki hiyo katika maendeleo ya jamii akibainisha kuwa changamoto za sekta ya elimu nchini kwa NMB ni jambo la kipaumbele kutokana na kwamba elimu ni uti wa mgongo wa taifa lolote duniani. “NMB tulipokea maombi kuwa mnahitaji stuli na meza za maabara,tulifarijika na kuamua kuja mara moja kushirikiana nanyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya elimu kwa watoto wetu katika shule hii”,alieleza. 
“Tunatambua kuwa kupitia jamii ndipo wateja wetu wengi wanapotoka,kwa hiyo kurudisha sehemu ya fai... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More