BENKI YA TPB Pls YAWEKA REKODI KIUTENDAJI, SASA MTAJI WAKE WAFIKIA SHILINGI BILIONI 60 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA TPB Pls YAWEKA REKODI KIUTENDAJI, SASA MTAJI WAKE WAFIKIA SHILINGI BILIONI 60

*Ofisa Mtendaji Moshingi aipongeza Serikali kwa uamuzi wa benki hiyo kuunganishwa na Twiga Bancorp
Na  Said Mwishehe, Blogu ya JamiiBENKI ya TPB Pls imesema imeweka rekodi nzuri ya utendaji katika kipindi cha miaka 6 iliyopita ambapo hadi sasa mtaji wake umeongezeka kutoka Sh. bilioni 8 mwaka 2010 hadi kufikia zaidi ya Sh.bilioni 60. 
Imefafanua aidha  kwa mwaka 2017, benki ya TPB ilitoa gawio la zaidi ya Sh. bilioni moja kwa Serikali ambaye ndiye mwenye hisa nyingi. 
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshingi wakati anatoa shukrani zake kwa Serikali kutokana na uamuzi wake wa kuamua kuiunganisha benki hiyo na pamoja na Benki ya Twiga Bancorp.
Akifafanua kuhusu benki hiyo amesema katika kuendelea kutekeleza majukumu yao benki ya TPB kwa mwaka 2017 ilipata faida kabla ya kodi ya Sh.bilioni 18.4 ikilinganishwa na faida ya Sh.bilioni 15.7 iliyopatikana mwaka 2016. 
Amesema matokeo hayo ya awali kwa robo ya kwanza ya mwaka 2018 inaonyesh... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More