Benki ya TPB yasaidia vifaa Taswa SC - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Benki ya TPB yasaidia vifaa Taswa SC

Na Mwandishi wetuBenki ya TPB imeendelea kuisadia  klabu ya  Waandishi wa habari za michezo  nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo ambavyo vitatumiwa na timu hiyo katika michezo yake mbalimbali.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja  Mawasiliano wa  Benki ya TPB Chichi Banda alisema kuwa wamesaidia msaada huo ni sehemu ya shughuli za Benki na kutambua mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari Nchini na muendelezo wao katika shughuli za kijamii ambapo mbali ya michezo, pia usaidia afya na elimu.
Chichi alisema kuwa wamefariji kakutoa msaada huo kwaTaswa SC ambayo mara kadhaa imekuwa ikitwaa ubingwa katika mashindano maalum ya vyombo vya habari yanayofanyika kila mwaka mkoani Arusha.
Alisema kuwa benki ya TPB ni wadau wakubwa wa michezo na mbali ya Taswa SC, pia usaidia timu nyingine.
“Waandishi wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, wameamua kuhamasisha michezo katika jamii, kwa vitendo, hii imetupa faraja kubwa sana kwetu, ”alisema Ch... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More