BENKI YA UBA YABORESHA HUDUMA ZA KIMTANDAO KWA KUZINDUA MAGIC BANKING - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BENKI YA UBA YABORESHA HUDUMA ZA KIMTANDAO KWA KUZINDUA MAGIC BANKING

Ikiwa ni jitahada za kuendelea kuwa benki bora Barani Afrika kwa huduma za simu za mkononi na kuendelea kuendana na jinsi mtandao unapokuwa haraka na kuwa na bidhaa na huduma zilizo bora kabisa, benki ya UBA Tanzania leo imetangaza kuzindua huduma nyingine bora ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70# kwa hapa Tanzania.

Huduma hii ya Magic Banking itamfanya mteja kwa kutumia simu yake ya mkononi kuweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hii ya Magic Banking, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Huduma za Kimtandao UBA Bank Tanzania Asupya Nalingigwa alisema kuwa mbali na huduma ya Magic Banking kufanya kazi kwenye simu aina yeyote ile lakini huduma hii ni salama, ya haraka na nafuu na mteja haitaji kuwa n... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More