BI.GAUDENSIA ATUA MKOA WA MJINI ZANZIBAR,ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BI.GAUDENSIA ATUA MKOA WA MJINI ZANZIBAR,ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Ndugu Gaudensia Kabaka amewataka Wanawake kuitumia vyema fursa ya Ujasiriamali ili wajiongezee kipato na kujiajiri wenyewe.

Rai hiyo ameitoa katika ziara yake katika Mkoa wa Mjini Kichama wakati akizungumza na Wana CCM huko katika ukumbi wa Kwa Waazee Sebleni Unguja.

Alisema ujasiriamali ni nyenzo pekee ya kuwakomboa wanawake kiuchumi na wakaweza kuwa na uwezo na nguvu za kujiajiri wenyewe.

Ameeleza kwamba CCM kwa sasa ipo katika Sera na Mkakakati wa Siasa na Uchumi hatua inayotakiwa kuchangamkiwa na Akina Mama Nchini, kwa kuanzisha vikundi vya ushirika.

Kupitia ziara hiyo aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwalea wazee katika mazingira bora yanayowawezesha kupata huduma zote za msingi za kijamii.

Alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapibduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa busara zake za kuendeleza mambo mbali mbali yaliyoasisiwa na Rais wa kwanza wa Zanzi... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More