BI. LULU NG'WANAKILALA ATEULIWA KUWA OFISA MKURUGENZI MKUU MPYA WA ASASI YA LSF - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BI. LULU NG'WANAKILALA ATEULIWA KUWA OFISA MKURUGENZI MKUU MPYA WA ASASI YA LSF

Na Mwandishi Wetu
Shirika la Legal Services Facility (LSF) jane limetangaza rasmi uteuzi wa Bi Lulu Ng’wanakilala kama Ofisa Mkurugenzi Mkuu mpya. Katika kutekeleza kazi hii, anachukua nafasi ya Bw Kees Groenendijk, ambaye ameongoza asasi hii tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011.
Bi Ng’wanakilala, ambaye ana Shahada ya Pili katika Sheria ya Kimataifa na Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Livraserpool nchini Uingereza na Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, amedhamiria kufanya mabadiliko ya kitaasisi lengo kuu likiwa ni kuifanya LSF kupanua wigo utoaji wa msaada wa kisheria kwa mamilioni ya wanaume na wanawake maskini Tanzania wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.
Anachukua uongozi wa asasi isiyo ya kiserikali ambayo imewezesha uwepo wa wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar, wanaotao msaada wa kisheria kwa watanzania wenye matatizo ya kisheria na kuwawezesha kupata haki zao.
Akitoa mtazamo wake, Afisa Mkurugenzi anayemaliz... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More