Biashara Zangu Ndio Zinanikondesha Sio Kingine-FaIza Ally - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Biashara Zangu Ndio Zinanikondesha Sio Kingine-FaIza Ally

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza kwa Mbunge wa Mbeya Mjini Sugu, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi kuwa kinachomkondesha kwa hivi sasa ni biashara zake.


Faiza ambaye amesuka gumzo baada ya kuonekana anapukutika mwili wake amedai kuwa anakonda kutokana na mizigo ya watu kuchelewa kufika kwa wakati.


Kwenye mahojiano yake na gazeti la  Ijumaa Wikienda, Faiza amesema kuwa watu wengi wanamzungumzia na kumshangaa jinsi alivyopungua, lakini hawajui ni jinsi gani hali wala halali usiku kwa sababu ya mizigo ya watu kuchelewa kufika bandarini.Watu wengi wananiuliza ninakondeshwa na nini, lakini hawajui ni jinsi gani ninakosa amani mizigo ya watu walioniagiza isipofika kwa wakati ninachanganyikiwa kabisa”.Faiza ni mmoja kati ya wajasiriamali wa Kwenye Instagram ambaye anafanya biashara ya Kukutwa watu vitu kutoka China kuja Tanzania.


 


The post Biashara Zangu Ndio Zinanikondesha Sio Kingine-FaIza Ally appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More