Biashara Ziliniokoa Muziki Ulipotaka Kunizika - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Biashara Ziliniokoa Muziki Ulipotaka Kunizika

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ally timbulo ameweka wazi kuwa Biashara zake za ufugaji wa kuku ndio zilimuokoa kimaisha pale ambapo Muziki ulitaka kumzika  kiuchumi.


Timbulo ameweka wazi biashara yake aliyoanzisha ya kufuga kuku ndio imemfanya mpaka hivi sasa hategemei pesa za shoo peke yake kama wasanii wengine.


Kwenye mahojiano na , Timbulo alifunguka kuwa, aliamua kujishughulisha na mambo ya ufugaji baada ya kuona hawezi kukaa tu na kusubiria shoo maana kuna wakati zinakata kabisa hivyo hata pesa ndogondogo inakuwa ni shida.Nina kuku 2,000 ambao nafuga na nina wauza kwa bei tofauti. Kuna wengine wanaanzia elfu 15 hadi elfu 40 kutegemeana na mbegu. Pia ninauza mayai, inanisaidia mimi na familia yangu”.Wasanii wengi wamekuwa wakiishi katika maisha magumu wakati wakiwa na majina makubwa katika jamii hali iliyopelekea wengi wao kugeukia Biashara nyingine mbali na muziki.


The post Biashara Ziliniokoa Muziki Ulipotaka Kunizika appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More