Billnas Adai Hawezi Kuwa na Mwanamke Anayejichubua - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Billnas Adai Hawezi Kuwa na Mwanamke Anayejichubua

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana BillNas ameibuka na kuweka wazi kuwa hawezi kuwa kwenye mahusiano ya Kimapenzi na mwanamke anayejichubua.


Billnas ameweka wazi kuwa Kitendo Cha mwanamke kubadilisha rangi yake ya mwili kutoka Kwenye weusi asilia kuwa mweupe anakuwa kama amejikataa mwenyewe.


Kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amekataa uhusiano na wanawake wanaotumia kitaulo (mkorogo):Kujichubua au kubadilisha rangi ya mwili sio pia kabisa mimi mwanamke anayejichubua siwezi kuwa naye kimapenzi uaani sijui iweje.


Kujichubua ni kitu ambacho mimi niko tofauti nacho sana kwa sababu kwanza unakataa uhalisia wako vile ambavyo mwenyezi Mungu amekubariki na hii rangi yetu nyeusi ipo very unique.


Lakini pia kuna vitu vingi vinavyomfanya mtu kuwa mzuri na viko ndani yako na sio muonekano wako wa nje Fanya matendo mema mazuri watu watakupenda”.Baada ya kuachia kibao chake kipya ‘Labda’ Bill Nas alitangaza kuwa video hiyo ilidukuliwa k... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More