BINTI WA GEORGE W. BUSH AOLEWA NA CRAIG COYNE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BINTI WA GEORGE W. BUSH AOLEWA NA CRAIG COYNE

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamiiBINTI wa kwanza wa aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush, Barbara Pierce Bush (36) amefunga pingu za maisha na Craig Louis Coyne (37) ambaye ni mwandishi na mtunzi  wa filamu katika harusi ya siri iliyohusisha familia siku ya jumapili huko Maine.
Barbara aliongozwa na baba yake George W. Bush  wakati akiolewa na Craig katika harusi ndogo iliyofanyika nyumbani kwao Kennebunkport Maine, Bush alieleza furaha yao (yeye na mkewe Laura) baada ya binti  yao kufunga ndoa na kumtakia kila la heri.
Wawili hao hawakuweka mahusiano yao wazi na imekuwa harusi ya kuduwaza wengi kwani walionekana kama marafiki wa muda mrefu.
Barbara ameeleza kuwa angetamani uwepo wa bibi yake na hiyo ilikuwa  zawadi kwa bibi yake na wajina wake Barbara Bush aliyefariki mwezi Aprili mwaka huu akiwa na umri wa miaka 92.
Katika ukurasa wake wa instagram bi. Laura Bush ameandika kuwa "Ilikuwa siku ya furaha kwa bintiye Barbara kufunga ndoa na mpenzi wake Craig na wamemfurahia kuwa seh... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More