BINTI WA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI GEORGE W. BUSH AOLEWA NA CRAIG COYNE



Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.
BINTI wa kwanza wa aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush, Barbara Pierce Bush (36) amefunga pingu za maisha na Craig Louis Coyne (37) ambaye ni mwandishi na mtunzi wa filamu katika harusi ya siri iliyohusisha familia siku ya jumapili huko Maine.
Barbara aliongozwa na baba yake George W. Bush wakati akiolewa na Craig katika harusi ndogo iliyofanyika nyumbani kwao Kennebunkport Maine, Bush alieleza furaha yao (yeye na mkewe Laura) baada ya binti yao kufunga ndoa na kumtakia kila la heri.
Wawili hao hawakuweka mahusiano yao wazi na imekuwa harusi ya kuduwaza wengi kwani walionekana kama marafiki wa muda mrefu.
Barbara ameeleza kuwa angetamani uwepo wa bibi yake na hiyo ilikuwa zawadi kwa ... Continue reading ->
Source: KajunasonRead More