Bobi Wine amlipua Kanye West ‘ameikosea sana Afrika kwa kusalimiana na Rais Museveni’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Bobi Wine amlipua Kanye West ‘ameikosea sana Afrika kwa kusalimiana na Rais Museveni’

Msanii wa muziki na Mwanaharakati nchini Uganda, Bobi Wine amemshukia vikali rapa Kanye West baada ya kukutana na Rais wa Taifa hilo Yoweri Museveni.


Image result for bobi wineBobi Wine

Bobi Wine akihojiwa na gazeti la The Guardian la Uingereza amesema kuwa Kanye amejidhalilisha sana kwa kutumia vibaya  picha yake nchini Uganda hii ni baada ya kukutana na Rais Museveni Jumatatu Ikulu nchini humo.


Limgekuwa jambo kubwa sana kama angetumia muda wake kutangaza viongozi wazuri barani Afrika lakini sio kukutana na Rais mwenye miaka 32 madarakani, anayeminya Demokrasia na kukandamiza vyama vya upinzani, ametukosea sana waafrika.“amesema Bobi Wine na kuendelea.


Pata picha mimi ni msanii lakini leo hii nazuiliwa kufanya tamasha ndani ya nchi yangu, kisa napingana na mawazo ya Rais halafu leo yeye anaenda kusalimiana naye,“.


Kanye West alikuwa nchini Uganda tangu wiki iliyopita akikamilisha baadhi ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya YANDHI.


SOMA ZAIDI – Kanye West na Kim Kardashian wakutana... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More