BOCCO AFUNGA MAWILI NA KUFIKISHA MABAO 100 LIGI KUU SIMBA SC YASHINDA 3-1 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BOCCO AFUNGA MAWILI NA KUFIKISHA MABAO 100 LIGI KUU SIMBA SC YASHINDA 3-1

Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
NAHODHA John Raphael Bocco amefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 wa mabingwa watetezi, Simba SC dhidi ya wenyeji, Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga – lakini akatolewa kwa kadi nyekundu.
Ushindi huo unarejesha amani Simba SC baada ya timu kucheza mechi mbili zilizopita bila kushinda, ikitoa sare ya 0-0 na Ndanda FC mjini Mtwara na kufungwa 1-0 na Mbao FC mjini Mwanza.
Simba SC sasa inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi tano kuelekea pambano dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Bocco ambaye atakosa mechi dhidi ya Yanga Septemba 30, alifunga bao la kwanza kwa penalti dakika ya 41 baada ya kiungo Shiza Kichuya kuangushwa na Miraj Maka kwenye boksi dakika ya 40.
Bocco akaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 100 kwenye Ligi Kuu tangu imeanzishwa mwaka 1996, baada ya kuifungia Simba SC bao la pili dakika ya 45, akimalizia pasi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe kufuatia krosi ya mshambul... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More