BOCCO AFUNGIWA MECHI TATU NA KUPIGWA FAINI YA SH. 500,000 KWA KUMCHAPA KONDE MCHEZAJI WA MWADUI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BOCCO AFUNGIWA MECHI TATU NA KUPIGWA FAINI YA SH. 500,000 KWA KUMCHAPA KONDE MCHEZAJI WA MWADUI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga ngumi mcheza wa Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Septemba 23, 2018 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 
John Bocco amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga ngumi mcheza wa Mwadui FC

Wambura amesema kwamba baada ya Bocco kutolewa kwa kadi nyekundu katika mechi hiyo namba 52, Simba SC ikishinda 3-1 yeye akifunga mabao mawili, adhabu nyingine ni kukosa mechi tatu na faini ya Sh. 500,000.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji na tayari Bocco amekwishakosa me... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More