Bocco aionya Kagera Sugar - Sports Kitaa | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Bocco aionya Kagera Sugar

John Bocco
NAHODHA wa Simba, John Bocco, amesema 'hawatapoa' kwenye mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Kagera Sugar huku akiwataka wapinzani wao hao kujiandaa kwa kipigo.
Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, inashuka dimbani kukamilisha tu ratiba, lakini ikiwa na lengo la kuweka rekodi ya kutopoteza mechi yoyote ya Ligi Kuu msimu huu kufuatia kuutwaa ubingwa huo mapema ikiwa imebakiza mechi tatu.Akizungumza na Nipashe jana, Bocco, alisema baada ya kutwaa ubingwa, lengo lao sasa nikuhakikisha wanamaliza michezo yao kwa ushindi."Tumefanya kazi kubwa tangu kuanza kwa msimu, hatutakuwa tayari kupoteza mchezo wakati tumebakisha michezo miwili tu," alisema nyota huyo mwenye mabao 14."Sisi lengo letu ni kushinda michezo yote iliyobakia kuanzia huu wa Jumapili na ule wa Songea (dhidi ya Majimaji) na tunauwezo wa kufanya hivyo," aliongeza kusema.
Alisema ubingwa wao walioutwaa hivi karibuni 'utapendeza zaidi' kama watafanikiwa kumaliza ligi bila kufungwa.Simba ilitanga... Continue reading ->


Source: Sports KitaaRead More