BODABODA, BAJAJI, TAXI KUSHINDWA KULETA HESABU NA KUKUSABABISHIA HASARA, NINI UFANYE KISHERIA. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BODABODA, BAJAJI, TAXI KUSHINDWA KULETA HESABU NA KUKUSABABISHIA HASARA, NINI UFANYE KISHERIA.

Na  Bashir  YakubSio siri wengi waliowekeza kwenye biashara ya bajaji,bodaboda,taxi na hata daladala wamejuta kufanya hivyo. Wengi wameingia hasara na mambo hayakuwa kama walivyotarajia. Na niamini,waliomo leo kwenye hiyo biashara sio wale walioanza, bali ni wageni kwani walioanza walishaacha siku nyingi kuepuka kichwa kuuma.Sasa yafaa tuzingatie mambo kadhaa ya kisheria ili kuona  namna gani unaweza kudhibiti biashara hii na hata ikikushinda isikushinde ukiwa mwenye kupoteza(looser).Katika kufanya hivyo tutizama mambo mawili, kwanza Mkataba, na pili Udhamini.1.MKATABA.Eneo la mkataba au makubaliano ni eneo muhimu  sana tangu unapowaza biashara hii. Mkataba ndiyo tafsiri ya uhusiano wako na huyo unayemkabidhi chombo. Popote, na wakati wowote mtakapotofautiana  rejea yenu ya kwanza ni mkataba. Mkataba ndio biashara yenyewe, na hivyo uimara wa mkataba utatambulisha uimara wa biashara, halikadhalika udhaifu wa mkataba huenda ukawa ndio udhaifu wa biashara.Na uimara wa mkataba ni seh... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More