BODI YA UTALII YAANDAA MAONESHO YA UTALII NCHINI YATAKAYOANZA OKTOBA 12 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BODI YA UTALII YAANDAA MAONESHO YA UTALII NCHINI YATAKAYOANZA OKTOBA 12

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.BODI ya Utalii Nchini (TTB) imeandaa maonesho ya kimataifa ya utalii yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo (SITE) ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba Jijini Dar es Salaam.
Lengo la maonesho hayo ni kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo na wakati wa utalii Tanzania pamoja na wafanyabiashara kutoka masoko makuu ya Utalii.
Akizungumza na waandishiw a haari kuelekea maonesho hayo yanayotarajiwa kuanza Oktoba 12 hadi 14, Mwenyekiti wa bodi wa TTB Jaji Mstaafu Maiko Miayo amesema kuwa, onesho hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na makampuni ya uoneshaji 170 kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika na Ukanda wa bahari ya Hindi pamoja na wafanyabiashara wa kimataifa na vyombo vya habari 300.
Jaji Miayo amesema mara ya kwanza maonesho hayo yalifanyika mwaka 2014 na yalihudhuriwa na waoneshaji kutoka makampuni 40 pamoja na wafanyabiashara na vyombo vya habari va kimataifa kutoka nchi 24.
Alisema, hawakuishia hapo mwaka 2015 maonesho hayo yalizidi kuvutia ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More