BODI YAZIONYA VIKALI ASHANTI, KILUVYA UNITED NA MASHUJAA KWA MAKOSA DARAJA LA KWANZA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BODI YAZIONYA VIKALI ASHANTI, KILUVYA UNITED NA MASHUJAA KWA MAKOSA DARAJA LA KWANZA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), maarufu kama Kamati ya Saa 72 imezionya klabu za Daraja la Kwanza, Ashanti United ya Dar es Salaam, Kiluvya United ya Pwani na Mashujaa ya Kigoma kwa makosa mbalimbali.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 
Wambura amesema kwamba Ashanti United na Kiluvya United zote zimepewa Onyo Kali kwa kutowasilisha orodha ya wachezaji wake katika kikao cha maandalizi ya mechi hiyo namba moja iliyomalizika kwa sare ya 1-1 Septemba 29 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. 
Wambura Mgoyo amesema adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
Na Mashujaa imeonywa kwa kuchelewa kufika uwanjani... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More