Bodigadi wa Floyd Mayweather atuma salamu za vitisho kwa Bondia McGregor na Khabib - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Bodigadi wa Floyd Mayweather atuma salamu za vitisho kwa Bondia McGregor na Khabib

Moja ya Mabodi wa Bondia wa Mwanamasumbwi, Floyd Mayweather ameahidi kumlinda mteja wake asiguswe wala kushambuliwa nje ya uwanja na mtu yeyote hata kama mtu huyo angekuwa mbabe kama Bruce Lee.


Video thumbnailJizz Mack

Akiongea na mtandao wa TMZ, Bodigadi huyo anayefahamika kwa jina la Jizz Mack, amesema kuwa kutokana na vurugu zilizotokea wiki mbili zilizopita katika ukumbi wa T-Mobile mjini  Las Vegas nchini Marekani, yeye kwa sasa ameimarisha zaidi ulinzi kwa mteja wake hasa katika kipindi hiki ambacho kuna uwezekano mkubwa wa Mayweather kupangiwa pambano na Bondia kutoka Urusi Khabib Nurmagomedov.


Haijalishi awe ni McGregor, awe ni Khabib au hata kama awe ni Bruce Lee mimi nitamdhibiti mara moja mtu yeyote atakayekuwa na lengo la kumshambulia mteja wangu nje ya uwanja.” amefunguka Mack.


Wiki mbili zilizopita, Bondia Khabib Nurmagomedov baada ya kumpiga McGregor aliruka nje ya ulingo na kuanza kusambaza kichapo kwa wapambe wa McGregor.


SOMA ZAIDI – Conor McGregor apokea kipigo cha karne ku... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More