Bondia aliyemdunda Muingereza: Niliondoka Tz kama mfungwa baada ya kunyimwa vibali - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Bondia aliyemdunda Muingereza: Niliondoka Tz kama mfungwa baada ya kunyimwa vibali

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ambaye wiki iliyopita aliitangaza vizuri bendera ya Tanzania kwa kumtwanga bondia wa Uingereza, Sam Eggington kwa T OK ndani ya dakika ya pili, amefunguka kuzizungumzia changamoto ambazo alizipata mapaka akafika Uingereza.


Hassan amedai aliondoka Tanzania bila support kutoka kwa Watanzania kwani hata kibali cha kwenda huko alikosa.


“Katika vitu sitavisahau ni kwamba mimi nilisafiri hapa kama mfungwa, nilikosa kibali na nikaondoka kama mkimbizi, nimeondoka mimi kwa kuazima ada ya mwanafunzi anasoma, tumekopa ada yake ya shule ili tukalipie VISA.,” Hassan aliwaambia waandishi muda mchache baada ya kutoka bungeni.


Aliongeza,”Hii imeniuma ingawa leo kila mtu anajitokeza na kusema yeye ni meneja wangu na nasikitika kusema sina Meneja yoyote,”


Wabunge wa Tanzania waliamua kumchangia bondia huyo ambapo kila mbunge aliamua kuchanga tsh 20,000 ili ajikimu ya maisha.The post Bondia aliyemdunda Muingereza: Niliondoka Tz kama mfungwa baada ya kunyimwa vib... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More